Kuhusu Sisi

Redio Ukweli 92.7 MHz ni kituo cha redio cha Kikatoliki kilichoanzishwa na Jimbo Katoliki la Morogoro mwaka 2000. Kwa zaidi ya miaka 20, redio hii imekuwa ikitoa huduma kwa jamii kwa utangazaji wa habari, elimu, burudani na maadili ya Kikristo.


Redio inajulikana kwa programu zake mbalimbali, zikiwemo Misa Takatifu kwa Kiswahili, habari za ndani na kimataifa, muziki wa Kikristo na wa kitamaduni, mafunzo ya Biblia na maadili, vipindi vya elimu na afya, na burudani kwa jamii..


Kauli Mbiu ya Redio Ukweli, “Ukweli utawapeni Uhuru,” inaonyesha dhamira ya redio ya kuelimisha na kuwawezesha watu kupata uhuru wa kweli. Redio inaamini kuwa maarifa ni nguvu, na kwamba watu wenye taarifa wanaweza kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao. Pia inapatikana katika tovuti ya radioukweli.or.tz.