Taa za umemejua zilivyosaidia kupunguza migogoro ya binadamu  na tembo katika kijiji cha Kanyenja mkoani Morogoro

Ukweli FM Podikasiti
Ukweli FM Podikasiti
Taa za umemejua zilivyosaidia kupunguza migogoro ya binadamu  na tembo katika kijiji cha Kanyenja mkoani Morogoro
Loading
/

Morogoro. Kuishi karibu na hifadhi ya wanyamapori, kwao imekuwa ni kilio kila siku. Hii inatokana na wanyamapori kuvamia na kufanya uharibifu wa makazi na mashamba yao.

Hawa ni wakazi wa Kijiji cha Kanyenja, Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ambao wanaishi karibu na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ambayo inasifika kwa idadi kubwa ya tembo. 

Tangu kijiji hicho chenye ukubwa wa kilomita za mraba 25,000 kianzishwe mwaka 1996, kimekuwa kikipata changamoto ya migogoro ya binadamu na wanyamapori hasa Tembo. 

Shughuli kubwa ya wakazi wa kijiji hiki ni kilimo cha mpunga na miwa ambapo tembo wamekuwa wakitoka hifadhini na kuingia mashambani ili kujipatia chakula.  

Suala hili limekuwa siyo tu likiwapa hasara wakazi hao, bali limekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu tembo huvamia pia makazi yao na wakati mwingine kuwajeruhi watu na kusababisha vifo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *