
Morogoro. Katika jamii za maisha ya Mtanzania kila mmoja ana namna yake ya kujiingizia kipato ili kupata mkate wa kila siku, wengine ni waajiriwa serikalini, Taasisi na sekta mbalimbali au makampuni lakini wengine hawana ajira rasmi za kuwaingizia kipato
Waokota taka chupa za plastiki ni Miongoni mwa kundi ambalo halina ajira rasmi ingawa wanajiingizia kipato na maisha yao yanasonga kila uchao.
Kundi hili ni moja kati ya kundi linalokutana na kadhia nyingi wanapopita katika mitaa mbalimbali kujikusanyia taka za plastiki hasa chupa za maji kama njia mojawapo ya kujiingizia kipato.
Licha ya kukiri kwamba hufanya kazi hiyo ili kusafisha mazingira pamoja na kujipatia kipato,hakuna anayewaamini wanachukuliwa kama wezi waliojificha chini ya mwavuli wa kukusanya taka