Vikoba vilivyo saidia kuboresha maisha ya wanawake waishio usharoba wa Nyerere Selous -Udzungwa

Ukweli FM Podikasiti
Ukweli FM Podikasiti
Vikoba vilivyo saidia kuboresha maisha ya wanawake waishio usharoba wa Nyerere Selous -Udzungwa
Loading
/

Morogoro. “Nimejenga kwa kutumia Vikoba, nimesomesha watoto wangu kupitia Vikoba na bado naendesha shughuli zangu ndogo ndogo za ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji kuku kupitia Vikoba, tunapata elimu ya uhifadhi kupitia vikoba”

“Tangu tulipoanza kikoba uharibifu wa msitu umepungua sana tofauti na awali watu walikuwa wanaingia msituni kutafuta kuni na kuuza, lakini kwa sasa nakopa kwenye kikoba na kumaliza kabisa shida zangu nasomesha watoto wangu ndio maana naona umuhimu wa kikoba na tunaomba waendelee kutusaidia”

Haya ni maneno ya  Hidaya Omary mama mjane wa miaka 52. Kikoba kimemsaidia kuendesha shughuli za ujasiliamari na kumuwezesha kupata fedha za kutunza familia na kusomesha watoto wake. 

Hidaya ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Magombera katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ni miongoni mwa wanachama wa kikundi cha kuweka akiba na kukopeshana cha Amani A.

Tangu ajiunge na kikundi hicho miaka 10 iliyopita, amepata ahueni ya maisha kwa sababu anajikimu mahitaji yake ya ndani ambapo awali ilikuwa kitendawili.

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Vikoba ni ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi.

Mfumo wa VICOBA unalenga kusaidia jamii zinazoishi katika hali ya umaskini na zenye kipato cha chini ili ziweze kujikwamua na umaskini hasa katika ngazi ya familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *