Na Angela Kibwana. Morogoro

Chama cha wafanyakazi wakatoliki Tanzania CWM, kimeungana na wanachama wote wa vyama vya wafanyakazi wa Kikristo ulimwenguni kuadhimisha siku ya kazi zenye staha ulimwenguni inayoadhimishwa Oktoba 07 kila mwaka duniani kote
Akizungumza kwa mahojiano maalum Bwana Pastor Nyoni mwenyekiti wa CWM Taifa ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho Jimboni Morogoro amesema maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika parokia ya Mtakatifu Paulo Matombo Jimboni Morogoro.
Aidha katika maadhimisho hayo ya siku zenye staha ulimwenguni CWM imetoa tamko la kupinga na kulaani kuibuka kwa mamlaka za vyama vyenye mrengo wa kulia ambayo vinakandamiza haki msingi za wafanyakazi.
Maadhimisho hayo kitaifa yalifanyika Jimboni Morogoro Oktoba 5 mwaka huu katika parokia ya Mtakatifu Paulo Matombo Jimboni humo, ambapo wanachama wa Cwm Tanzania kutoka parokia mbalimbali walishiriki kikamilifu kwa ajili ya maadhimisho hayo
Bwana Nyoni amesema kuwa siku ya kazi zenye staha ulimwenguni, Cwm Tanzania itaendelea kusimama kidete kuhakikisha inaungana na wanachama wote kulaani vitendo vinavyoendelea kukandamiza wafanyakazi kufurahia haki zao za kibinafsi na kazi zenye staha

“Kuwadanganya watu na kudharau binadamu na kujidhuru, kunarudia onyo la Yesu Kristu katika Injili ya Mathayo 18: 6-7 yeyote atakayemkosesha mmoja wa wadogo hawa waniaminio, ingekuwa afadhali kwake kufungwa jiwe kuu la kusagia shingoni mwake na kuzamishwa katika kilindi cha bahari, ole wake ulimwengu kwa majaribu na kutenda dhambi” amesema Nyoni.
Hata hivyo amesema kuwa Cwm Tanzania itaendelea kukuza haki za kijamii na kiuchumi kwa wanachama wake kwa kuzingatia imani Katoliki

Ameongeza kuwa ili kukuza haki za kijamii na kiuchumi kwa maisha ambayo utume huo unasimamia kwa kuzingatia imani katoliki utazingatia tu endapo kama kila mwanamke au mwanamke atapata kazi nzuri yenye malipo yanayofaa yaani pesa taslimu au bidhaa, usalama kazini pamoja na mazingira ya kufanya kazi
Katika maadhimisho hayo wanachama wa CWM, wameshiriki kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa na wahitaji, parokiani Matombo ikiwa ni pamoja na kushiriki zoezi la kupanda miti kuunga mkono juhudi za kutunza mazingira.
Aidha katika ziara hiyo parokiani Matombo wametembelea vivutio mbalimbali ikiwemo kujua asili ya neno Matombo na kutembelea Jiwe lenye matiti ambalo ndio asili ya neno Matombo, pamoja na kufahamu historia ya msalaba wa Matombo.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka 2024 , “ Kazi kwa ajili ya kukuza haki za kijamii na kiuchumi kupitia imani katoliki