CWM yadhamiria kuboresha mahusiano kati ya waajiri na wafanyakazi majumbani.

Na Angela Kibwana, Morogoro.

Chama cha wafanyakazi wakatoliki Tanzania Cwm Jimboni Morogoro wameanzisha mpango mkakati wa kutoa semina kwa waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani ili kujenga mahusiano baina ya wafanyakazi na waajiri wao kuimarisha usawa katika ajira kwa kuzingatia haki na wajibu kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Cwm imefikia adhma hiyo kutokana na msingi wa nne wa chama hicho ambao unalenga kuwasemea wasio na sauti ya kujisemea (To be the voice of the voiceless) baada ya kuona changamoto zinazojitokeza kati ya waajiri na wafanyakazi wa majumbani ikiwemo kukosekana haki sawa kwa mfanyakazi na wajibu kwa mwajiri katika mazingira ya kazi.

Mafunzo hayo yanahusisha makundi ya vyama mbalimbali vya kitume ambapo kwa awamu ya kwanza semina ilitolewa kwa Semina hii inatolewa kwa makundi mbalimbali ambapo kundi la kwanza ilikuwa ni kwa wanawake wakatoliki Tanzania na wanachama wa CWM Dekania ya Kihonda na Dekania ya mjini pamoja na wajumbe kadhaa wa UWAKA

Disemba 17 mwaka huu 2024 CWM imetoa mafunzo kwa kundi la pili ikihusisha kwa mapadre wa Jimbo Katoliki Morogoro na ikiwemo viongozi dini mbalimbali kupaza sauti katika nyumba za Ibada, Maafisa maendeleo, Pamoja na viongozi wa mitaa ili kuwa mabalozi wa kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani.

Baadhi wa mapadri wa Jimbo Katoliki Morogoro wakishiriki semina iliyotolewa na CWM

Kwa kutambua msingi wa Kanisa Katoliki kumhudumia mwanadamu kimwili na Kiroho, CWM wamewashirikisha mapadri kwa sababu licha ya wao kujikita katika huduma zao za kiroho lakini wanaajiri wafanyakazi wa majumbani ambao wanatekeleza majukumu ya shughuli zote za nyumbani, kupika, kufua, kusimamia shughuli za kilimo na ufugaji ikiwemo kusimamia shughuli mbalimbali za kitaasisi katika dini

Lengo la Pili la kuwashirikisha mapadri na viongozi wa Kidini ni kupewa elimu namna ya kujua sheria wakati wa kushughulikia migogoro au kutoa stahiki za wafanyakazi wa majumbani mara baada ya kuacha au kuachishwa kazi, lengo la pili ni kuhakikisha wanatumia nyumba zao za ibada kuwasemea wafanyakazi wa majumbani kutokana na nyanyaso wanazokutana nazo kwa waajiri.

Kwa mujibu wa Victor Mackyao ambaye ni mwanasheria na mwezeshaji wa mafunzo hayo anasema Wafanyakazi wa majumbani ni nguzo muhimu katika maisha ya familia nyingi, wakitoa huduma zinazowezesha watu wengine kushughulikia majukumu yao ya kitaaluma na kijamii.

Ameongeza kuwa Wafanyakazi hao kimsingi wanatekeleza majukumu mengi ya msingi, kama vile usafi, uangalizi wa watoto, na maandalizi ya chakula, huku mara nyingi wakifanya kazi katika mazingira yasiyo na uwiano mzuri wa haki za kijamii na kiuchumi.

Pamoja na mchango wao mkubwa, bado kundi hili linakumbana na changamoto za msingi, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira rasmi, ujira mdogo, na mara nyingine ukosefu wa heshima na ulinzi wa kisheria.

Ndugu Victor amesema Sheria Namba 6 ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, inatoa mwongozo wa haki na wajibu kwa waajiri na waajiriwa,hivyo waajiri wanapaswa kufahamu na kutii sheria na taratibu zinazohusu ajira ya wafanyakazi wa majumbani.

Kadhalika kifungu cha 37 cha sheria hiyo ya ajira na mahusiano kazini kinatoa aina za makosa ambayo yanaweza kusababisha mfanyakazi kuachishwa kazi ikiwemo utovu wa nidhamu, wizi, kukosa uwezo, kutohitajika kazini kwa sababu mbalimbali.

Ameongeza kuwa kifungu cha 39 cha sheria hiyo kinamtaka mwajiri athibitishe uachishaji kazi kwa kufuata utaratibu ambapo wafanyakzi wengi wa nyumbani wamekumbwa na changamoto hii na kukosa haki zao msingi kwa kutoijua sheria na mahala salama pa kusemea.

Hata hivyo amesema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo inakusudia zaidi katika utatuzi wa masuala yanayohusu wafanyakazi wa majumbani ambapo washiriki wanajifunza uwezeshaji unaohusu haki na wajibu kwa lengo la kujenga mahusiano bora kwa waajiri na wafanyakazi wa majumbani

,,Hawa wafanya kazi wa majumbani wamekuwa na changamoto nyingi mojawapo ni kutokutambulika kama wanavyotambulika wafanyakazi wengine, pili jamii haiwapi thamani kwamba ni kundi muhimu ndani ya jamii, ndio maana wakati mwingine wanakuwa na tabia ya kufanya visasi baada ya kuwepo kwa changamoto zinazosababishwa na waajiri wao,, Amesema Mackyao.

Amesema kuwa wafanyakazi wa majumbani wana haki ya kuwa na mikataba ya ajira inayojumuisha maslahi yao, ujira na masaa kazini ili kujenga jamii iliyosalama kwa kuheshimiana kwa kuzingatia haki ya kulindwa, kupendwa na kuthaminiwa na jamii au waajiri wao.

,,Waajiri wanapaswa kuweka ratiba inayoeleweka na kuhakikisha wafanyakazi hao wa majumbani wanapata muda wa kupumzika ikiwemo haki ya kupata likizo, kadiri ya makubaliano ndani ya mkataba kati ya mwajiri na mfanyakazi wa nyumbani,, ameongeza Victor. 

Kufuatia tangazo la serikali namba 687 la mwaka 2022 ambalo ni maboresho ya tangazo la serikali namba 183 la 2011 inatoa viwango vya mishahara kulingana na sekta husika kwa mfanyakazi anayofanyia kazi ambapo wafanyakazi wa majumbani nao wakiwa ni kundi mojawapo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo mfanyakazi wa nyumbani ni mojawapo ya sekta inayotambulika kisheria ambapo mfanyakazi anayefanya kazi kwa mtu wa kawaida bila kuishi kwenye kaya ya mwajiri  anapaswa kulipwa kiasi cha shilingi 120,000 na mfanyakazi anaeishi na mwajiri uja na wakwatika òoanapaswa kulipwa.

Naye bwana Pastor Nyoni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania katika Mradi wa kuboresha mahusiano ya ajira kati ya waajiri na wafanyakazi wa Majumbani unaolenga kuboresha haki, wajibu na kukuza mchango wa wafanyakazi wa majumbani kuhakikisha wanatambuliwa, kuheshimiwa na kulindwa ipasavyo.

Kwa mujibu wa Bwana Pastor Nyoni, Wafadhili wa mradi huo ni KAB German na Germany Embassy Tanzania lengo ikiwa ni kuwezesha upatikanaji wa elimu inayosaidia mwajiri kutambua wajibu na haki za mfanyakazi wa nyumbani ambao wengi wao hawana uelewa kutambua haki zao.

,,CWM imeamua kuendesha semina kwa kutambua changamoto wanazopitia wafanyakazi wa majumbani pamoja na migogoro inayotokana  na changamoto za kutolipwa stahiki zao, kumekuwa na matukio mbalimbali kama vile vipigo na vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto ambapo ukifuatilia inasababishwa na mgogoro kati ya mwajiri na mfanyakazi,, Amesema Nyoni.

Victor Mackyao mwanasheria mwezeshaji wa CWM akitoa semina hiyo kwa mapadri wa jimbo la Morogoro

Kwa upande wake Mukhsin Mohamed  Imam Msikiti wa Kichangani Mkoani Morogoro akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini amewashukuru CWM akisema semina hiyo imeongeza wigo kwa viongozi wa dini kutetea wafanyakazi wa majumbani ambao kimsingi wengi wao wananyanyasika.

Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Kilakala amesema kuwa wenyeviti wa mtaa wameshuhudia kesi nyingi zinazowakabili wanyakazi ikiwemo kuajiriwa katika umri mdogo na wakati mwingine kusafirishwa kama biashara haramu watoto wanapakiwa kama mizigo na anapofika kwa mwajiri haki zake kusiginwa.

John Daud Kiyungi Afisa maendeleo Kata ya Kilakala Mkoani Morogoro amepongeza elimu iliyotolewa katika semina hiyo akiahidi kuichukua kama ajenda kuizungumzia katika baraza Kata ndani ya mitaa 15 ya kata hiyo ili wenyeviti wote wa mitaa kuifanyia kazi kutoa elimu kwa jamii ndani ya Kata husika

Naye Mwanasheria wa Jimbo Katoliki Morogoro Padri Methodi Maghali amekiri kwamba kumekuwepo na changamoto hizo migogoro kati ya waajiri na wafanyakazi katika maeneo na vijijini akisema kwamba mkakati wa Jimbo ni kuelimisha wakristu kutambua umuhimu wa mikataba kupunguza kesi zinazoweza kuibuka mfanyakazi kumshitaki Padri au Jimbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *