Matukio mbalimbali ya picha Sherehe ya UWAKA Jimbo Katoliki Morogoro

Askofu Lazarus Msimbe sds wa Jimbo Katoliki Morogoro akitoa baraka ya kuanza kwa adhimisho la misa takatifu sherehe ya kumuenzi somo wa Utume wa Wanaume Wakatoliki (UWAKA) Jimbo la Morogoro.

Askofu Msimbe akifukizia ubani katika altare tayari kwa kuanza adhimisho la misa Takatifu ya somo wa UWAKA Jimbo la Morogoro Juni 23,2024 katika Seminari ndogo ya Mtakatifu Petro.

Wanaume Wakatoliki Jimbo la Morogoro na baadhi ya waamini wengine waalikwa wakiwemo Wanawake Wakatoliki Jimboni humo wakifuatilia adhimisho la misa Takatifu linaloongozwa na Mhashamu askofu Lazarus Msimbe SDS.

Askofu Lazarus Msimbe akikata utepe kuzindua mpango kazi wa Utume wa Wanaume Wakatoliki wa miaka mitatu 2024-2027 katika ukumbi wa Seminari ndogo ya Mtakatifu Petro.

Baadhi ya picha za matukio mbalimbali yaliyoambatana katika sherehe ya somo wa Utume wa Wanaume Wakatoliki Jimbo la Morogoro Juni 23,2024 Seminari ndogo ya Mtakatifu Petro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *