Na Angela Kibwana
Morogoro
Naibu waziri wa uchukuzi David Kihenzile amesema ujenzi wa SGR unaashiria juhudi za serikali ya Tanzania kuboresha miundombinu na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa kwa kupunguza muda wa safari na kuongeza fursa za kibiashara.
Amesema hayo wakati akitoa salamu za serikali akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya jubilei ya miaka 25 ya upadre wa Padre Dr Liston Lukoo mkuu wa idara ya Katekesi Baraza la maaskofu Katoliki Tanzania Tec Iliyofanyika Melela Jimboni Morogoro.
Amesema kuwa kwa takwimu za wiki iliopita zimeonesha kwamba abiria takribani laki 380,000 wametumia huduma treni ya mwendokasi kutoka Dar es salaam, Morogoro hadi kufika jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Kihenzile, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ana dhamira thabiti ya kuboresha sekta ya uchukuzi na maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Hata hivyo Serikali pia inafanya mazungumzo ya mwisho kuunganisha Tanzania na Burundi kupitia mtandao huu wa reli, lengo kuu likiwa ni kuwezesha usafiri wa haraka na wa uhakika kwa wananchi.
Huduma ya SGR, imekuwa mkombozi wa kiuchumi na kijamii, kwa kuongeza matumaini mapya kwa Watanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
Mwisho.