Wadau wa uchaguzi hakikisheni wananchi morogoro wanajiandikisha

Morogoro

Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi jaji Jacob Mwambegele amewaomba wadau wa uchaguzi vyama vya siasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia vyombo vya habari na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wananchi mkoani Morogoro kujiandikisha katika zoezi la maboresho katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kushiriki kwenye zoezi la uchaguzi mkuu wa 2025.

Jaji Mwambegele ametoa OMBI hilo katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani uliofanyika katika ukumbi wa magadu mkoani Morogoro.

Akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo jaji Mwambegele amesema kuwa wadau hao ni muhimu kushiriki moja kwa moja kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi katika zoezi Hilo ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwa kuzingatia kuwa linatoa fursa ya kushiriki kwenye uchaguzi.

Nao baadhi ya wadau washiriki wa mkutano huo akiwemo peter Kapinga  Mjasiriamali kijana amewaomba vijana wenzake kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo muhimu kwa Taifa

Miongoni mwa wadau washiriki wa mkutano asasi za kiraia na vyama vya siasa wameeleza kuwa wataenda kutumia elimu walioipata kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa zoezi hilo kwa mustakabari wa uchaguzi tarajiwa.

Wadau wa uchaguzi mkoani Morogoro wakimsikiliza mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Taifa Jaji Jacob Mwambegele akifungua mkutano wa wadau ha oleo februari 17,2025 uliofanyika katika ukumbi wa Magadu mkoani Morogoro

Akifunga mkutano huo mjumbe wa tume hiyo balozi Omar Ramadhan Mapuri amesema ni vyema wadau katika kipindi hiki wakazingatia sheria zinazoongoza zoezi hilo

Mkoa wa morogoro unatarajia kuanza zoezi la uboreshaji na uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia macho moshi hadi saba mwaka huu.

Washiriki wa mkutano wa wadau wa uchaguzi wakisikiliza mawasilisho ya mada mbalimbali namna ya kwenda kuhamasisha uboreshaji na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga linalotarajiwa kufanyika kuanzia machi mosi hadi saba mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *