Wananchi Morogoro tumieni haki yenu ya kujiandikisha daftari la wapiga kura

Na Frank Castory

Morogoro

Mkurugenzi wa uchaguzi tume huru ya taifa ya uchaguzi Bwana Kailima Ramadhan amewataka wananchi mkoani morogoro kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kuboresha na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza machi mosi mwaka huu mkoani humo

Mkurugenzi Kailima ametoa wito huo leo februari 20,2025 wakati akizungumza na radio ukweli katika kipindi maalum kuhusiana na zoezi la uboreshaji na uandikishaji litakalofanyika mkoani humo kwa siku saba kuanzia machi mosi hadi saba katika vitongoji, vijiji na mitaa yote mkoani humo

Amesema kuwa suala la kufanya maboresho na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni muhimu kwa kila mwananchi mwenye sifa wakiwemo kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea

Aidha mkurugenzi huyo wa uchaguzi amewaomba wadau wote wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa dini, vyama vya siasa, vijana, wenye mahitaji maalum , vyombo vya habari na wengineo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi hilo muhimu kwa taifa

Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bw Kailima Ramadhani akizungumzia umuhimu wa wananchi wa Morogoro kujitokeza kuboresha na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia Machi 01-07,2025 katika studio za Radio Ukweli Februari 20,2025

Mkoa wa morogoro ni mkoa wa 30 kuendeshwa zoezi la uboreshaji na uandikishaji katika daftari la wapigara kura tangu kuzinduliwa mwaka na waziri mkuu Kassimu Majaliwa mnamo mwezi julai mwaka jana ambapo tume huru ya uchaguzi inatarajia kuandikisha wananchi laki tatu na elfu mbili katika mkoa wa morogoro kwenye zoezi hilo

Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bw Kailima Ramadhani akizungumzia na mtangazaji Frank Castory umuhimu wa wananchi wa Morogoro kujitokeza kuboresha na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia katika studio za Radio Ukweli Februari 20,2025

Kwa mwaka 2020 jumla wananchi 1,612,952 mkoani Morogoro walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura , ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni “KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *